Katika hali isiyo ya kawaida mzee mwenye umri wa miaka 75, Athuman Mchambua, mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ally jijini Dar es Salaam amezua gumzo mtaani baada ya kuamua kutafuta mke kwa kuweka bango barabarani.
Katika bango aliloliweka katikati ya barabara Mzee Mchambua alianisha sifa tano za mke anayemtaka pamoja na namba za simu za kuwasiliana naye.
Sifa hizo ni pamoja na awe mshika dini, uvumilivu wa ndoa, uwezo wa kilimo, apendo wa mume, watoto na wajukuu pamoja na usafi wa hali ya juu.
Mzee Mchambua ambaye alizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC Swahili) hivi karibuni alisema alifanya uamuzi huo baada ya kufiwa na mke wake aliyezaa naye watoto 11 na kumwacha akiwa hana mtu wa kumsaidia kutunza familia na kufanya shughuli za shambani.
Post a Comment